HALI SI HALI MWAMBONU SECONDARY SCHOOL

Shule hii imekuwa si shule tuu bali pia ni shule ya mapenzi na ngono za kiholela. Wakaazi wa maeneo ya shule hii na wazazi wa shule hii wamekemea vikali tabia chori kutoka kwa walimu.

Duru zinasema kuwa baadhi ya walimu wa shule hii wanaramba asali ya wanafunzi bila kujali umri wala maisha ya baadae ya wanafunzi hao. Hii si kinyume tu kulingana na sheria za mwajiri wa walimu TSC, bali ni kinyume pia kulingana na sheria za nchi na katiba ya Kenya. Ni hatia kwa mtu mzima kulala na msichana ambaye hajafikisha miaka kumi na nane.

Tabia hii mbaya imekita mizizi katika shule hii ya Mwamonu Secondary School.

Duru zinazidi kusema kuwa, mwaka huu wanafunzi kadhaa wamefanya mtihani wa kidato cha nne wakiwa waja wazito. Washukiwa wakuu wa kutekeleza mradi huo wa kupachika wanafunzi mimba wakiwa ni walimu wao.

Kawaida walimu huchukuliwa kama watu wa kuonyesha mifano njema katika jamii na kuelekeza watoto kukua wakiwa na maadili mema ila kwa shule hii mambo ni kinyume kabisa.

Cha kusikitisha zaidi ni kuwa ripoti kama hizi ziliripotiwa tangu mwaka jana na kufikia sasa hakuna hatua yoyote imechukuliwa hivyo kuwafanya walimu hawa majadingili kuona kuwa wanavyofanya ni kawaida.

Mnamo tarehe 27 Julai, mwaka Jana, mwalimu Mkuu aliandika MEMO kukemea swala hilo ila kufukia sasa hakuna hatua yoyote imechukuliwa.

Kama wazazi na wakaazi tumlaumu nani? Ni shirika la TSC limelalia kazi ama ni Mwalimu Mkuu?

Duru zinazidi kusema kuwa walimu hao wanaojihusisha na usherati huu wamekuwa wazembe kazini, hata syllabus za masomo yao zinawashinda kumaliza. Hii inatuma wanafunzi kutofanya vizuri kwenye mitihani yao ya mwisho.

Kama wakaazi na wazazi tunaomba shirika husika lichukue hatua kali haraka iwezekanavyo kabla hatujaanza kuchukua sheria mikononi.

Orodha ya walimu tuliowamulika ni kama ifwatavyo.

1. Chief Principal
2. Madam Mutua (deputy Principal)
3. Mwalimu Getate
4. Mwalimu Wasike
5. Mwalimu Ongweso

Tunaomba ikiwezekana watano hawa wasikanyage Mwambonu Secondary School Januari mwaka ujao.

Tukiwaona tutachukua hatua kama jamii kuhakikisha wamechukuliwa hatua za kisheria na waliopachika watoto wetu mimba wamechukuwa majukumu ya mimba zao.

Ni hayo kwa sasa.

AHSANTE KWAELA NEWS NETWORK kwa kuangazia.

https://www.facebook.com/share/p/15TvLyjwn7/

Comments

Be the first to add a comment